Kenya Yaendelea Kurekodi Visa Vya Covid-19 Miezi 6 Baadaye

  • 4 years ago
Ni takriban miezi sita tangia kisa cha kwanza cha corona kutangazwa nchini. Licha ya virusi hivi kusababisha maambukizi na hata vifo, swala la iwapo kenya imekabiliana na virusi hivi ipasavyo linaendelea kuwakanganya wakenya huku wengi wakilegeza kamba katika vita hivi. Lakini wizara ya afya imeonya kuwa kuna hatari ya wimbi la pili la maambukizi iwapo sheria zilizowekwa hazitafuatiliwa.haya yanajiri ambapo watu wengine 188 wameambukizwa huku watatu wakifariki.

Recommended