Baraza Maalum Laanza Mazungumzo Ya Kufungua Maeneo Ya Ibada

  • 4 years ago
Wakenya watalazimika kungoja wiki tatu zaidi ili kujua iwapo wataruhusiwa kurejea katika maeneo ya ibada. Akizundua mkutano wa baraza maalum la viongozi wa kidini litakaloandaa mwongozo wa kufanikisha mjadala huo, waziri wa maswala ya ndani daktari Fred Matiang'i amewataka viongozi hao kuwa na lengo katika majadiliano yao ili kupata suluhu la kudumu. Mwenyekiti wa baraza hilo askofu mkuu anthony muheria amesema iwapo wakenya watafuata maelekezo yaliyotolewa na wizara ya afya ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, hivyo basi mpango huo utafanikishhwa.