Mahakama Kuamua Hatma Ya Mchakato Wa BBI Leo Alasiri
  • 3 years ago
Mahakama Kwa Sasa Inatoa Uamuzi Ambao Utatoa Mwelekeo Kuhusu Mchakato Wa Marekebisho Ya Katiba Kupitia Mchakato Wa BBI. Jopo La Majaji Joel Ngugi, George Odunga, Jarius Ngaah, Janet Mulwa Na Chacha Mwita Wamepangiwa Kutoa Uamuzi Wao Kuhusu Maombi Saba Yanayopinga Mchakato Wa BBI. Mnamo Mwezi Februari, BBI Ilipata Pigo Kubwa Baada Ya Mahakama Kuu Kuizuia Iebc Kuanzisha Mipango Ya Kura Ya Maamuzi Kuhusu Mswada Wa Marekebisho Ya Katiba. Katika Uamuzi Uliotolewa Na Jopo La Majaji Watano, Tume Huru Ya Uchaguzi Na Mipaka Ilisimamishwa Kwa Muda Kujiandaa Kwa Kura Ya Maamuzi Na Inasubiria Kusikilizwa Na Kuamuliwa Kwa Maombi Saba Yaliyowasilishwa Kupinga Mchakato Huo.
Recommended